• KEVIN DE BRUYNE ANGEWEZA KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI



    Kiungo Mshambuliaji Wa Manchester City Kevin De Bruyne Amefunguka Na Kusema Kuwa Mama Yake Alizaliwa Barani Afrika Nchini Burundi Lakini Alipofikisha Umri Wa Miaka Saba Aliondoka Na Babu Yake Kwenda Nchini England Kwaajili Ya Masomo.

    Lakini Pia Mama Yake Huyo Anayejulikana Kwa Jina La Anna De Bruyne Ameishi Nchini Ivory Coast , De Bruyne Mwenyewe Amezaliwa Katika Mji Wa Drongen, Ghent Huko Nchini Ubelgiji Belgium.


    De Bruyne Anazungumza  Kiholanzi, Kifaransa, Kijerumani Na Kiingereza, Katika Mahojiano Ya Mwaka  2013, De Bruyne Alisema: "Mama Yangu Ana Asili Ya Kiingereza  , Lakini Mimi Ni Mbelgiji Kikamilifu."  Kutoka Mjini Drongen,  Sehemu Ya Kiholanzi Inayozungumza Kibelgiji.


    Mbelgiji Huyo Anashikilia Rekodi Ya Kuwa Mchezaji Aliyetoa Pasi Nyingi Za Magoli Tangu Alipojiunga Na Manchester City Na Kuanza Kuitumikia Timu Hiyo September 2015 Akiwa Na Assist 33 Nafasi Ya Pili Ikishikiliwa Na Kiungo Wa Spurs Christian Eriksen Mwenye Assist 29 Sawa Na Mesuit Ozil Wa Arsenal Mwenye Assist 29 David Silva Wa Manchester City Mwenye Assist 20 Sawa Na Cesc Fabregas Wa Chelsea Mwenye Assist 20 Kwenye Ligi Ya England  Na Msimu Huu Wa 2017/2018 Ameshatoa Pasi 6 Za Magoli Katika Michezo 10 Na Kufunga Goli 1.


    Kuhusu Uchezaji Wake Ndani Ya Uwanja De Bruyne Anasema Anapenda Kucheza Katika Nafasi Ya Anayocheza Hivi Sasa Manchester City Namba 10 Akiwa Na Kiungo Wa Kihispania David Silva Na Anajifunza Vitu Vingi Sana Kutoka Kwake Kwani Silva Ni Mchezaji Aliyekamilika Na Anauwezo Mkubwa Sana.

    Akizungumza na Mwandishi wa Sportsmail Jamie Redknapp , De Bruyne Amesema  ' Tangu Niungane Na  Pep Guardiola Naona Nacheza Aina Ya Mpira Ninaoupenda   Na Hii Ni  Aina Ya Mpira Ambao Unapendwa Na Wachezaji Wote , Kila Mmoja Anakaa Kwenye Nafasi Yake Na Inakuwa Rahisi Kuifanya Timu Icheze Kama Ambavyo Tunafanya , Kufunga Magoli ni Vizuri Lakini Kutoa Pasi za Magoli ni Kitu Bora Zaidi Kwangu '.

     


  • You might also like

    No comments:

    Post a Comment

Powered by Blogger.

Blog Archive