• PAUL POGBA AREJEA KIKOSINI KUIVAA CHELSEA KESHO



    Kiungo Wa Manchester United Paul Pogba Amejiunga Na Timu Yake Hiyo Kwenye Mazoezi Katika Uwanja Wa Carrington Mapema Hapo Jana Kujiandaa Na Mchezo Wa Ligi Ya England Dhidi Ya Chelsea Utakaopigwa Siku Ya Jumapili Ya November 5 Katika Dimba La Stanford Bridge.
    Paul Pogba Akiwasili Katika Uwanja wa Mazoezi wa Manchester United Carrington.

    Pogba ‘24’ Alipata Majeraha Kwenye Mchezo Dhidi Ya Fc Basel Klabu Bingwa Ulaya Na Kushindwa Kuitumikia Timu Yake Kwenye Michizo 11 , Lakini Kiungo Huyo Anatarajiwa Kurejea Kisosini Wikiend Hii Baada Ya Kuanza Mazoezi Na Wachezaji Wenzake. 

    Mchezo Wa Hapo Kesho United Itawakosa Fellaini, Michael Carrick, Zlatan Ibrahimovic Na Marcos Rojo Ambao Bado Wanauguza Majeraha Yao Na Kocha Jose Mourinho Amesema Anapata Wakati Mgumu Kutokana Na Majeruhi Lakini Anaamini Wachezaji Wake Watapata Matokeo Japo  Kuwa Mchezo Huo Utakuwa Mgumu.


    Kuelekea Mchezo wa Kesho Chelsea na Manchester United wanaingia katika mchezo wa Jumapili katika kupunguza pengo la pointi dhidi ya Vinara wa ligi Manchester City , Kocha Jose Mourinho Anarudi Katika Dimba lake la Nyumbani la Zamani Baada Kujiunga na United katika kipindi cha kiangazi cha mwaka 2016 Akitokea Chelsea . 

    Amekuwa na Rekodi ya Kushinda mechi 5 kati ya 9 dhidi ya vilabu alivyowahi kuvifundisha katika maisha yake ya ukocha, amefungwa mechi 3 na sare 1.Ushindi wa 1-0 dhidi ya Benfica ugenini ulimaliza mfululizo wa kupoteza mechi za ugenini dhidi ya vilabu vyake vya zamani. 

    Chelsea wanaingia katika mchezo wa Jumamosi wakiwa wana rekodi ya kupoteza mechi 1 tu kati ya 15 walizocheza vs United katika uwanja wa Stamford Bridge. Wameshinda 9 na kutoa sare 5. Msimu uliopita walimtandika Mourinho 4-0 darajani.

    Taarifa za Majeruhi
    Chelsea – Bakayoko mwenye majeruhi ya groin, David Luiz (paja), Hazard (achilles), Kanté (hamstring), Morata (match fitnes) – wana hati hati ya kucheza.

    Manchester United – Majeruhi Fellaini (goti), Pogba (hamstring, wote wanatarajia kurudi 18 Nov), Ibrahimovic (goti, Dec), Carrick (calf, unknown)

  • You might also like

    No comments:

    Post a Comment

Powered by Blogger.

Blog Archive